Pablo hajafurahishwa na sare ya Yanga

Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema hajafurahishwa na sare ya bila kufungana tuliyopata dhidi ya Yanga kwa kuwa lengo letu lilikuwa tupate pointi zote tatu.

Pablo amesema alama tatu zingetufanya kuwasogolea zaidi lakini matokeo ya leo yamewafanya wapinzani kuwa karibu na ubingwa ingawa hatutakata tamaa mpaka mwisho.

Akiuzungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema ulikuwa mzuri uliotawaliwa na mbinu ingawa tulipaswa kutumia vizuri nafasi tulizopata.

Pablo ameongeza kuwa hatuna muda wa kupumzika kwa kuwa maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Namungo siku tatu zijazo yanapaswa kuanza mara moja.

“Sijafurahishwa na matokeo ya sare, tuliingia uwanjani kwa dhamira ya kutafuta ushindi kwakuwa tunahitaji kupunguza tofauti iliyopo na bado tunahitaji kutetea ubingwa wetu.

“Tunacheza mchezo ujao ugenini dhidi ya Namungo siku tatu zijazo kwa hiyo tunajiandaa na safari ingawa hatuna muda wa kutosha wa maandalizi ya mechi,” amesema Pablo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER