Okrah ni Mwekundu na Mweupe

Klabu yetu imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji Augustine Okrah kutoka Bechem United inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ghana kwa mkataba wa miaka miwili.

Okrah (28), ana uwezo wa kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani ikiwemo winga zote mbili na kucheza nyuma ya mshambuliaji.

Katika msimu uliopita Okrah akiwa na Bechem amecheza mechi 31 akifunga mabao 14 na kutoa assist nane.

Kwa takwimu hizo zinaonyesha Okrah ni mfungaji hodari licha ya kucheza kama kiungo mshambuliaji kitu ambacho kimetuvutia na kusafiri hadi nchini Ghana kuifuata saini yake.

Okrah kwa nyakati tofauti amewahi kuzitumikia timu za Asante Kotoko (Ghana), Al Marreikh, Al Hilal (zote za Sudan) Smouha FC (Misri) na North East United (India)

Okrah ameitumikia timu ya taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 20 mwaka 2013 ambapo mwaka 2019 aliitwa kwa mara ya kwanza timu ya taifa ya wakubwa ya Ghana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER