Mwinuke aelezea furaha ya kufunga bao lake la kwanza

Winga, Jimmyson Mwinuke amefunguka kuwa amejisikia furaha kufunga bao lake la kwanza akiwa na jezi yetu tangu ajiunge nasi mwanzoni mwa msimu.

Mwinuke alifunga bao hilo safi dakika ya 70 likiwa ni la sita kati ya saba tuliyowafunga Ruvu Shooting baada ya kupokea pasi ya upendo kutoka kwa Clatous Chama akiwa ndani ya 18, ikiwa ni dakika tatu tangu aingie uwanjani.

Mwinuke amesema anaamini kadiri atakavyoendelea kupata nafasi ya kucheza ataisaidia timu kupata ushindi kama alivyofanya jana.

“Namshukuru Mungu na nimekuwa na furaha kwa kufunga bao lile, naamini kadiri ninavyozidi kupata nafasi inaniongezea kitu kwenye majukumu ya kuitumikia Simba.

“Mwalimu bado ananipa nafasi na nadhani najitaidi kufuata kile anacho niagiza, matumaini yangu ni kuwa mashabiki wataendelea kuwa na furaha sababu timu yetu inaendelea kuimarika,” amesema Mwinuke.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER