Kocha Mkuu Juma Mgunda amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi Mei.
Mgunda amewapiku Miguel Gamondi wa Yanga na Bruno Ferry wa Azam ambao alikuwa anashinda nao katika kinyang’anyiro hicho.
Katika mwezi Mei, Mgunda ametuwezesha kushinda mechi sita kati ya saba tuliyocheza na kukusanya pointi 19.
Mechi hizo ni dhidi ya Mtibwa (2-0), Tabora United (2-0), Azam FC (3-0), Geita Gold (4-1), KMC (1-0), JKT Tanzania (2-0), Kagera Sugar (1-1),