Kocha Mkuu Fadlu Davids ameongoza mazoezi ya asubuhi kwa mara ya kwanza tangu achukue nafasi hiyo.
Fadlu ametua kambini jana jioni akiwa na wasaidizi wake na moja kwa moja leo ameanza kukiongoza kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Katika mazoezi ya leo wachezaji walianza kukimbia uwanja mara kadhaa ili kurejesha utimamu wa mwili kutokana na kutoka kwenye mapumziko.
Baada ya zoezi hilo wachezaji walifanya mazoezi mbalimbali ya kucheza mpira uwanjani huku wakipewa maelekezo kutoka kwa Fadlu na wasaidizi wake.