Kikosi kuingia kambini leo, waliokuwa Stars warejea

Kikosi chetu kinaanza kambi rasmi leo jioni kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa Aprili 3, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Wachezaji watakaoingia kambini ni pamoja na nyota wetu 10 waliokuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichocheza mechi mbili za kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Equatorial Guinea na Libya.

Nyota wengine Thaddeo Lwanga aliyekuwa anatumikia kikosi cha Uganda (The Cranes) na Joash Onyango wa Kenya (Harambee Stars) wao wanatarajiwa kutua nchini muda wowote kuanzia sasa ambapo watajiunga na wenzao moja kwa moja kambini.

Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema wachezaji 19 wataingia kambini leo baada ya mazoezi ya jioni yatakayofanyika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena, Bunju jijini Dar es Salaam.

“Timu itaingia kambini leo kujiandaa na mchezo Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita na wachezaji wetu waliokuwa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania tayari wamerejea huku wale wa kimataifa wakianza kurejea leo na wengine kesho,” amesema Rweyemamu.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER