Kikosi chetu leo saa 10 jioni usiku kitashuka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuikabili KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kaimu Kocha Mkuu Juma Mgunda amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho dhidi ya Geita Gold siku tatu zilizopita.
Mgunda amewaanzisha Ayoub Lakred, Sadio Kanoute na Willy Onana kuchukua nafasi za Hussein Abel, Pa Omar Jobe na Edwin Balua.
Hiki hapa kikosi kamili kilivyopangwa:
Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Fabrice Ngoma (6), Ladaki Chasambi (36), Mzamiru Yassin (19), Saido Ntibazonkiza (10), Sadio Kanoute (8), Willy Onana (7)
Wachezaji wa Akiba:
Hussein Abel (30), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Abdallah Hamis (13), Babacar Sarr (33), Edwin Balua (37), Saleh Karabaka (23), Luis Miqussone (11), Clatous Chama (17).