Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Kagera Sugar

Kikosi chetu leo saa 10 jioni kitashuka katika Uwanja wa Kaitaba kuikabili Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kocha Juma Mgunda amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kile kilichocheza mchezo wa mwisho dhidi ya Azam FC.

Mgunda amemuanzisha Babacar Sarr kuchukua nafasi ya Fabrice Ngoma anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Hiki hapa kikosi kamili kilichopangwa:

Ayoub Lakred (40), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Babacar Sarr (33), Edwin Balua (37), Mzamiru Yassin (19), Freddy (18), Sadio Kanoute (8), Ladaki Chasambi (36).

Wachezaji wa Akiba

Hussein Abel (30), Feruz Teru (31), David Kameta (3), Hussein Kazi (16), Shomari Kapombe (12), Willy Onana (7), Abdallah Khamis (13), Saleh Karabaka (23), Pa Omar Jobe (2).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER