Simba Queens itashuka katika Uwanja wa Abebe Bikila saa 9:45 mchana kuikabili FAD Djibouti katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kocha Mkuu Juma Mgunda ameweka wazi kuwa malengo ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ili kuibuka mabingwa.
Hiki hapa Kikosi Kamili kilichopangwa:
Caroline Rufa (18), Fatuma Issa (5), Wincate Kaari (12), Ruth Ingosi (20), Violeth Nicholas (26), Ritticia Nabbosa (13), Elizabeth Wambui (4), Vivian Corazone (17), Jentrix Shikangwa (25), Precious Christopher (8), Amina Bilal (11).
Wachezaji wa Akiba
Gelwa Yonah (21), Dotto Evarist (2), Easther Mayala (23), Daniela Ngoyi (22), Saiki Mary (19), Jackline Albert (16), Mwanahamisi Omary (7), Shelda Boniface (9), Asha Rashid (14).