Kibu afanya maajabu jioni kwa Mkapa

Bao la kichwa la dakika ya mwisho lililofungwa na Kibu Denis limetuwezesha kupata pointi tatu muhimu nyumbani dhidi ya CS Sfaxien baada ya ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kibu amefunga bao hilo dakika ya mwisho ya nyongeza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na kiungo mkabaji, Yusuph Kagoma.

Mshambuliaji Hazem Haj Hansen aliipatia CS Sfaxien bao la kwanza dakika ya tatu baada ya mlinzi Che Fondoh Malone kurudisha pasi fupi kwa mlinda mlango.

Kibu alitupatia bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Jean Charles Ahoua.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi huku Sfaxien wakitumia muda mwingi kujiungusha na kupoteza muda.

Mabadiliko aliyofanya kocha Fadlu Davids kipindi cha pili ya kuwaingiza Valentine Nouma, Kagoma, Joshua Mutale na Steven Mukwala yaliongeza kasi na kutufanya kuongeza mashambulizi mengi langoni mwa Sfaxien.

X1. Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 77′), Che Malone (Chamou 64′), Hamza, Fernandez (Kagoma 64′), Kibu, Ngoma, Ateba (Mukwala 45′), Ahoua (Mutale 64′), Awesu

Walioonyeshwa kadi: Che Malone 57′ Kibu 90+9

X1: Aymen, Nasraoui (Koume 45′), Conte, Hazem (Habboubi 55′), Achref (Baraket 55′), Derbali, Pedro, Dhaoui (Becha 71′), Baccar, Sakouhi (Traore 71′) Layouni

Walioonyeshwa kadi: Habboubi 63′ Aymen 66′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER