Kauli ya Mgunda kuelekea mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar

Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa kesho saa 10 jioni yamekamilika.

Mgunda amesema pamoja na nafasi mbaya walioyopo Mtibwa bado haitakuwa mechi rahisi kwetu na tumejiandaa kuwakabili.

Mgunda amesema kuwa Mtibwa ni timu nzuri na inatengeneza nafasi nyingi kwahiyo tutaingia kwa tahadhari zote kwakuwa lengo letu ni kuchukua pointi zote tatu.

“Hii ni Ligi na hakuna timu dhaifu. Mtibwa ni timu bora na tunaiheshimu na tumejiandaa kuhakikisha tunapata pointi tatu.

“Siku zote kwenye kila mchezo kunakuwa na mazuri na mabaya yale mazuri tunayaongeza na mapungufu tunayapunguza au kuyaondoa kabisa, tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Mgunda.

Akizungumzia hali ya kikosi Mgunda amesema kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amefungiwa mechi tatu lakini kuna nyota wengine ambao wanaweza kuziba nafasi yake.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER