Kagere, Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Namungo leo

Nyota Medie Kagere na Chris Mugalu wataongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa mwisho wa ligi kuu msimu huu wa 2020/21 dhidi ya Namungo FC utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni.

Katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Azam FC, Kagere alifunga bao la kusawazisha baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Mugalu hivyo leo Kocha Didier Gomes ameamua kuwaanzisha pamoja.

Mlinda mlango Aishi Manula amerejea langoni huku Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wakirejea kwenye nafasi zao za ulinzi wa pembeni.

Ibrahim Ame atacheza na Pascal Wawa kwenye beki wa kati wakati Erasto Nyoni akichukua nafasi ya Taddeo Lwanga kwenye kiungo wa ulinzi.

Viungo washambuliaji Clatous Chama, Luis Miquissone na Rally Bwalya watakuwa na kazi moja ya kurahisisha kazi ya Kagere na Mugalu.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (15), Mohamed Hussein (15), Ibrahim Ame (5), Pascal Wawa (6), Erasto Nyoni (18), Clatous Chama (17), Rally Bwalya (8), Medie Kagere (14), Chris Mugalu (14), Luis Miquissone (11).

Benchi

Beno Kakolanya (30), David Kameta (27), Gadiel Michael (2), Joash Onyango (16), Kennedy Juma (26), John Bocco (22), Hassan Dilunga (24).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER