Hitimana: Tumecheza kwa presha kubwa

Kaimu Kocha Mkuu Hitimana Thierry, amesema katika mchezo wa leo dhidi ya Polisi Tanzania tulicheza kwa presha lakini tunashukuru kwa kupata alama tatu muhimu.

Hitimana amesema kitendo cha kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na mabadiliko makubwa ya benchi la ufundi yalisababisha wachezaji kucheza kwa presha.

Hitimana ameongeza kuwa katika mchezo wa leo wapinzani wetu wa kwanza walikuwa sisi wenyewe na Polisi walikuwa wa pili lakini kikubwa tumepata ushindi.

“Tumetoka kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na tumebadili benchi la ufundi kwa hiyo tulikuwa na presha kubwa ndiyo maana nasema wapinzani wetu wa kwanza walikuwa sisi wenyewe,” amesema Hitimana.

Kuhusu mabadiliko ya wachezaji wanne katika kikosi yametokana na baadhi ya nyota wetu katika eneo la kiungo kuwa majeruhi.

“Taddeo Lwanga ni majeruhi na Jonas Mkude hakuwa fiti asilimia 100 ndiyo maana tumefanya mabadiliko yale kikosini ingawa nilitamani kuanza na washambuliaji wawili lakini kikubwa tunafurahi kwa ushindi,” amesema Hitimana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER