Bwalya: Naipenda nchi yangu lakini Simba kwanza

Kiungo mshambuliaji Rally Bwalya, amesema atajitoa kuhakikisha anaisaidia timu yetu kufanya vizuri dhidi ya Red Arrows kesho ili kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika licha ya kucheza kwenye ardhi ya nyumbani kwao Zambia.

Bwalya amesema Simba ni waajiri wake na siku zote ataipa nafasi ya kwanza katika kila kitu kama mkataba wake unavyoeleza.

“Ninasikia furaha kucheza katika ardhi ya nyumbani, naipenda nchi yangu lakini nimekuja kikazi nitahakikisha naisaidia Simba kupata ushindi ili tuingie hatua ya makundi,” amesema Bwalya.

Akizungumzia mchezo wa kesho Bwalya amesema itakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

“Kama alivyosema kocha, mechi itakuwa ngumu, tunajua Red Arrows wataingia kwa nguvu kutafuta mabao lakini sisi ni Simba tutakuwa tayari kuwakabili,” amesema Bwalya.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER