Bocco: Matokeo ya jana yametushtua

Nahodha John Bocco ameweka wazi kuwa matokeo ya mchezo wa jana dhidi ya watani wetu Yanga yametushtua na tunatakiwa kujipanga kuelekea msimu mpya wa ligi.

Bocco amesema ingawa hatujategemea kupoteza kama ilivyo kwa mashabiki wetu walivyodhani lakini imedhihirisha ligi itakuwa ngumu.

Bocco amewashukuru mashabiki wetu waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutuunga mkono ingawa matokeo hayakuwa upande wetu.

Mfungaji huyo wa muda wote wa ligi kuu amesema kwa sasa tunahamishia nguvu katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Biashara United ambao utapigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Karume mkoani Mara.

“Mchezo dhidi ya Biashara utakuwa mgumu, Biashara ipo kwenye kiwango bora kwa sasa lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kurudisha imani ya mashabiki,” amesema Bocco.

Kikosi chetu kimeondoka jioni hii kuelekea jijini Mwanza ambapo kitapumzika na kesho asubuhi kitaelekea mkoani Mara.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER