Barbara: Mashabiki tufuate masharti ya CAF mechi na AS Vita

Licha ya kuruhusiwa kuingiza mashabiki 10,000 kwenye mchezo wetu wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa Jumamosi, Mtendaji Mkuu wa Klabu, Barbara Gonzalez amewasisitiza mashabiki kufuata masharti yaliyotolewa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Akizungumzia mchezo huko utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, Barbara amesema CAF imetoa masharti mengi ambayo yanahusiana na kujikinga na janga la homa ya mapafu (COVID 19).

Barbara ametaja baadhi ya masharti hayo ambayo ni lazima kuvaa barakoa, lazima kuacha nafasi ya viti vitatu kati ya mtu na mtu na hakutaruhusiwa kuuzwa tiketi uwanjani.

“Kama tukishindwa kufuata hata moja tutasababisha nchi kufungiwa tena kuingiza mashabiki uwanjani katika mechi zetu.

“Tumeruhusiwa kuingiza mashabiki 10,000 uwanjani lakini tumepewa masharti mazito na kama tukishindwa kuyafuata tutafungiwa tena.

“Ninachowaomba mashabiki tufuate taratibu zilizowekwa ni faida kwetu Wanasimba  na taifa kwa ujumla tunapaswa kuwa mfano sababu ndiyo timu ya kwanza kucheza baada ya kufunguliwa,” amesema Barbara.

Viingilio kwenye mchezo huo mzunguko vitakuwa Sh 10,000, VIP B Sh 25,000 na VIP A Sh 40,000.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER