Alichosema Kocha Mgunda kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Namungo

Kocha Msaidizi Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

Mgunda amesema tunafahamu mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Namungo hasa tukijua wapo nyumbani lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

Mgunda ameongeza kuwa licha ya uchovu wa safari wachezaji wote waliopo kikosini wapo tayari kwa mchezo wa kesho na tunafahamu haitakuwa rahisi.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, maandalizi ya yamekamilika wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, tunawaheshimu Namungo ni timu nzuri ina wachezaji bora na wapo nyumbani haitakuwa rahisi lakini tupo tayari,” amesema Mgunda.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER