Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mgunda amesema maandalizi ya mchezo wa kesho wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya JKT Tanzania utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa yamekamilika.
Mgunda amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wetu JKT kutokuwa kwenye nafasi nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
Mgunda amesema ni mchezo muhimu kwetu kupata pointi tatu ambazo zitatuweka kwenye mazingira mazuri ya kumaliza nafasi mbili za juu huku tukisubiri matokeo ya timu nyingine.
Mgunda ameongeza kuwa kesho ni siku ya mwisho ya kufunga pazia la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 kila mchezo utakuwa mgumu na kila timu inahitaji kupata ushindi.
“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na timu ipo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunashinda mchezo wa mwisho ili tupige hesabu zetu tukiwa na alama tatu,” amesema Mgunda.